Mkutano wa mazingira COP21 waanza Ufaransa

Image caption Mkutano wa mazingira COP21 waanza Ufaransa

Viongozi wa dunia wanaanza mazungumzo muhimu ya wiki mbili yanayonua kufikia makubaliano ya kudhibiti ongezeko la joto duniani.

Rais wa Ufaransa Fran├žois Hollande,amesema hali ya baadaye ya binadamu iko hatarini na kuonya kuwa serikali zitalaumiwa iwapo viongozi watakosa kuchukua fursa hii kufanya maamuzi muhimu.

Hatahivyo mwandishi wa BBC anasema ahadi zilizotolewa hazifikii viwango vinavyohitajika ili kupunguza kiwango cha joto duniani kwa nyuzi mbili.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amesema nchi zilizoendelea zinapaswa kupunguza viwango vya joto zaidi kuliko nchi masikini.

Rais Barrack Obama ameungana na viongozi wengine mjini Paris Ufaransa kwa mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani ambao unanuiwa kuafikiana kuhusu viwango vipya vya kuzuia uchafuzi wa mazingira.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano

Viongozi hao watahutubia mkutano huo baadaye hii leo kabla ya wajumbe kutoka zaidi ya nchi mia moja themanini kujaribu kuafikiana mkataba mpya katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Alipowasili, Obama alielekea moja kwa moja hadi kituo cha burudani cha Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi wiki mbili zilizopita.

Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

Wakati huohuo ,afisa mmoja mwandamizi katika ujumbe wa Iran, katika mazungumzo ya umoja wa mataifa mjini Paris, ameiambia BBC kuwa taifa lake litapunguza uzalishaji wa hewa chafu inayochafua mazingira kwa kiasi kikubwa wakati vikwazo vilivyowekewa taifa lake vitakapoondolewa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Obama na Xi Jinping wamekutana katika mkutano huo mjini Paris

Makamu wa rais Masoumeh Ebtekar, ambaye ni kiongozi wa idara ya mazingira nchini Iran amesema, taifa lake litakuwa na uwezo wa kuagiza mafuta safi isiyochafua mazingira.

Amesema tangu mkataba wa nuklia kuafikiwa na mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani, julai mwaka huu, mataifa kadhaa ya ulaya na kampuni zimeonyesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa nishati isiyochafua mazingira ikiwa kuzalisha umeme kutumia miale ya jua au Solar.