Waisraeli waliochoma moto Mpalestina kuhukumiwa

Image caption Mohammad Abu Khdair alitekwa nyara na kuuawa Jerusalem

Mahakama moja nchini Israel imewapata waisraeli wawili na hatia ya kumuua kijana wa kipalestina mwaka wa 2014.

Washtakiwa hao wawili hawakutajwa kwa majina kwani wana umri mdogo.

Image caption Wakili wa Yosef Ben David anasema huenda anamatatizo ya kiakili

Mashtaka ya mshukiwa wa tatu ambaye anatajwa kuwa ndiye aliyepanga mauaji hayo yameahirishwa ilikuruhusu uchunguzi wa kiakili.

Kijana mwenye umri wa miaka kumi na sita Mohammed Abu Khadair alichomwa moto akiwa hai mwezi julai mwaka jana baada ya kutekwa nyara Mashariki mwa Jerusalem.

Image caption Wazazi wake wamelalamikia 'uongo'' dhidi ya mtuhumiwa mkuu

Mauaji hayo yalikuwa yakulipiza mauaji ya waisraeli watatu katika Ukanda wa Mgharibi.

Mauaji hayo yalikuwa mojawapo ya visa vilivyosababisha vita vya Gaza.