IMF kuidhinisha Yuan kuwa sarafu ya kimataifa

Haki miliki ya picha AP
Image caption IMF kuidhinisha Yuan kuwa sarafu ya kimataifa

Shirika la fedha duniani IMF linatarajiwa kutangaza baadaye kuwa sarafu ya uchina ya Yuan, itajumuishwa kwenye orodha ya sarafu za kimataifa.

Hatua inayoashiria kukua kwa umuhimu wake katika mfumo wa uchumi wa dunia.

Utawala wa Beijing umekuwa ukitaka sarafu ya Yuan kuwa na hadhi sawa na sarafu za dola ya Marekani, Euro, Yen ya Japan na Pauni ya Uingereza na umeaweka weka mageuzi kadhaa ya kiuchumi ili kuleta mabadiliko.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachanganuzi wanasema Uchina,sharti iwe tayari kuwa wazi zaidi kuhusu jinsi inavyoendesha masoko yake ya kifedha .

Hata hivyo wachanganuzi wa kiuchumi wanasema kwa sarafu hiyo ya Yuan kuwa sarafu ya kimataifa, Uchina ni sharti iwe tayari kuwa wazi zaidi kuhusu jinsi inavyoendesha masoko yake ya kifedha .