Uturuki yadaiwa kuwa na ushirika na IS

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Urusi, Vladmir Putin akihutubia jijini Paris

Urusi imeshutumu Uturuki kwa kuishambulia ndege yake ya kivita karibu na mpaka wake na Syria ili kulinda biashara yake ya mafuta na Wanamgambo wa IS.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi jijini Paris, Rais wa Urusi, Vladmir Putin amekiita kitendo cha kuangushwa kwa Ndege yake kuwa ni ''kosa kubwa''

Uturuki imekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa IS na kudai kuwa wao ni sehemu ya Operesheni inayoongozwa na Marekani inayotekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo.

Serikali ya Uturuki imekataa kuomba radhi kutokana na tukio hilo.

Rubani mmoja raia wa Urusi alipoteza maisha na wengine kuokolewa kufuatia tukio la mashambulizi ya tarehe 24 Mwezi Novemba.

Uturuki imedai kuwa Ndege ya Urusi iliingia kwenye anga yake, madai amabayo Urusi imepinga.