Burkina Faso yapata Rais mpya

Roch Marc Christian Kabore Haki miliki ya picha
Image caption Rais Mteule alikua Waziri Mkuu wa zamani katika utawala wa Blaise Compaore

Roch Marc Christian Kabore ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alipata alisimia 53 nukta tano hivyo amepata ushindi wa moja kwa moja, kwa kuzoa zaidi ya asili mia 50.

Huu ndio uchaguzi mkuu wa kwanza tangu maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais wa miaka mingi Blaise Compaore.

Uchaguzi Mkuu ulitarajiwa kufanyika mwezi uliopita lakini ukacheleweshwa na jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu hapo mwezi Septemba.

Bwana Compaore anaishi uhamishoni katika nchi jirani ya Ivory Coast.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Mteule {Katikati/mwenye miwani} aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu

Mshindani mkuu wa bwana Kabore, Zephrine Diabre alipata asili mia 21 ya kura. Yeye ni Waziri wa zamani wa Uchumi na Fedha.

Duru zinasema bwana Diabre amekubali kushindwa na kumpongeza Rais mteule,Roch Marc Christian Kabore.