Syria: Ujerumani kuiunga mkono Ufaransa

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Chancellor, Angela Merkel

Baraza la mawaziri nchini Ujerumani limeidhinisha msaada kwa Ufaransa katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State .

Mpango huo sasa utahitaji kupata idhini ya bunge kabla ya utekelezaji. Ujerumani inatarajiwa kutoa msaada wa ndege za kivita, meli ya kivita na wanajeshi wapatao elfu kumi na wawili. Hatahivyo wanajeshi hao hawatahusika katika makabiliano ya moja kwa moja.

Hatua hiyo imechululiwa baada ya Chancellor, Angela Merkel, kukubali kutimiza ombi la msaada kutoka kwa Ufaransa kutokana na mashambulio ya kigaidi yalioyofanyika mjini Paris mwezi uliopita.