Cameroon 'yaua' wapiganaji 100 wa Boko Haram

Haki miliki ya picha
Image caption Wizara ya ulinzi nchini Cameroon imesema majeshi ya serikali yameua takriban wafuasi 100 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Nigeria Boko Haram.

Wizara ya ulinzi nchini Cameroon imesema majeshi ya serikali yameua takriban wafuasi 100 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Nigeria Boko Haram.

Wizara hiyo imesema kuwa mateka 900 wamekombolewa.

Operesheni hiyo ya siku tatu kuanzia Novemba tarehe 26- 28 kaskazini mwa nchi hiyo.

Idadi hiyo hata hivyo haijathibitishwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wizara hiyo imesema kuwa mateka 900 wamekombolewa.

Huku hayo yakiarifiwa takriban watu tisa wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanyika kwa wakati mmoja nchini humo.

Inashukiwa kuwa mashambulio hayo yamefanywa na wanamgambo wa Boko Haram .

Washambuliaji wawili walijilipua katika eneo la Waza Kaskazini mwa nchi karibu na mpaka wa Nigeria.

Haki miliki ya picha Screengrab
Image caption Cameroon ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki juhudi za kieneo kukabiliana na wanamgambo hao.

Wapiganaji wa Boko Haram wameimarisha harakati zao katika maeneo ya mipaka nchini Cameroon, Niger na Chad.

Cameroon ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki juhudi za kieneo kukabiliana na wanamgambo hao.