Majeshi ya China yalinda amani Sudan Kusini

Image caption Majeshi ya China yanalinda amani chini ya nembo ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini

Uchina imeanza kutuma mamia ya wanajeshi wake kwenda nchini Sudan Kusini mapema mwaka huu kujiunga katika kikosi cha umoja wa mataifa nchini humo ambacho ni kikosi cha kwanza cha Urusi katika mpango wa kulinda amani nje ya nchi.

Akiwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara barani afrika, China hufanya zaidi makubaliano ya kibiashara badala la kulinda amani katika bara hilo.

Uhusiano wa biashara ya mafuta wa China na Sudan Kusini ambalo ni taifa changa zaidi barani Afrika na ni jambo linalofanyika chini kwa chini.

Wanajeshi hao 1,031 wa umoja mataifa wanawajumuisha wataalamu wa afya na wahandisi.

Kuwepo kwao mjini hakutambuliki isipokuwa tu kwenye lango lao kuu lililoandikwa herufi za kichina.

Wakifahamika kama CHN-BATT, kikosi hicho cha China kimeitwa kutatua mizozo ndani ya kambi za wakimbizi ambazo zitatoa makao kwa zaidi ya watu millioni moja.

Image caption Wakifahamika kama CHN-BATT, kikosi hicho cha China kimeitwa kutatua mizozo ndani ya kambi za wakimbizi

Ripoti ya kamati ya umoja wa mataifa inayohusika na vikwazo ilisema kuwa makampuni ya China yalipeleka mizinga, bunduki ,,risasi na makombora kwenda nchini Sudan Kusini vyenye gharama ya dola milioni 20. Uuzaji wa silaha uliripotiwa kusitishwa kabla ya uasi wa mwishoni mwa mwaka 2013 lakini China ina uhusiano wa kiuchumi na Sudan Kusini na ndio inautetea.

Kikosi hicho cha China kimehitajika kuamua makabiliano baina ya makundi hasimu mara kadha haswa katika kambi ya wakimbizi.

Zaidi ya wenyeji milioni moja wanaishi kambini baada ya kutoroka makwao vita vilipotibuka desemba mwaka wa 2013.

Wanajeshi hao kwa kiasi kikubwa wanashughulikia maswala ya kiafya muundo msingi kulinda wahudumu wenza na hata kugawa maji masafi.

China kimsingi hapa inalenga kuvutia raia wa Sudan Kusini.

Image caption China kimsingi hapa inalenga kuvutia raia wa Sudan Kusini.

Kila baada ya muda wanajeshi wanatangamana na wenyeji wakipiga picha nao na kuwafunza lugha zao.

Majuzi ripoti maalum ya Umoja wa mataifa ililaumiwa kwa kuiuzia Sudan kusini silaha kali za kijeshi.

Kulingana na mchambuzi wa maswala ya kiuchumi James Shikwati'China haijakuja Afrika kupigana, wala majeshi yao hayana nia yeyote ya kufyatua risasi ila kulinda muundo msingi wa uchumi wake.

Bwana shikwati anaelezea mfano wa meli na manuari za kivita za China zinazolinda bahari ya Somalia

''Je unadhania wamekuja huko kuwapiga risasi maharamia ? La wamekuja kulinda njia zinazopitisha bidhaa kutoka China na zile zinazoelekea huko.'' anasema Shikwati

Bila shaka rais Xi Jinping amegutuka kufuatia mashmbulizi ya kigaidi ya hivi punde .

Inatarajiwa kuwa swala hilo litazungumziwa katika mkutano wa rais huyo wa China na viongozi wa mataifa ya Afrika huko Johannesburg baadaye wiki hii.