Cheche Uingereza mjadala wa kuivamia IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cheche Uingereza mjadala wa kuivamia IS

Wabunge nchini Uingereza wamegombana katika mjadala kuhusu mpango wa serikali kujiunga katika harakati za pamoja za kijeshi zinazoongozwa na Marekani kupambana na wanamgambo wa Islamic State ndani ya Syria.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amelitaja kundi hilo kama tishio kubwa kwa usalama wa taifa.

Cameron amesema kuwa mashambulizi dhidi ya kundi hilo yataisaidia Uingereza kuwa salama.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Cameron amesema kuwa mashambulizi dhidi ya kundi hilo yataisaidia Uingereza kuwa salama.

Hata hivyo Kiongozi wa upinzani , Jeremy Corbyn, amesema mabomu ya Uingereza yataua raia wasio na hatia.

Amesema wananchi wa Syria wangetaka mzozo huo kutatuliwa kwa njia ya amani na kwamba ana hamu ya kuona wakimbizi wa Syria waliopiga kambi barani Ulaya wakirejea nyumbani.

Baada ya mjadala, wabunge watapiga kura kuidhinisha au kupinga mpango huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesifia juhudi za David Cameron na kuelezea matumaini kuwa wabunge wataidhinisha mpango huo.

Image caption Kiongozi wa upinzani , Jeremy Corbyn, amesema mabomu ya Uingereza yataua raia wasio na hatia

Awali Cameron alishurutishwa kuomba radhi kwa wabunge baada ya kusema wale wanaopinga mashambulizi makali dhidi ya Islamic state wanaiunga mkono kundi hilo.

Baada ya mjadala huu wa saa 10 wabunge wataamua iwapo majeshi ya Uingereza yatajiunga na Ufaransa Marekani na Urusi.