Kituo cha redio kimechomwa moto Zanzibar

Image caption Kituo cha redio kimechomwa moto Zanzibar

Kituo kimoja cha radio kimechomwa moto na watu wasiojulikana huko visiwani Zanzibar.

Kituo hicho kijulikanacho kama 'Hits FM' ni maarufu kwa matangazo ya habari na vipindi vyengine.

Kuchomwa kwake hata hivyo kuinaibua taharuki haswa katika kipindi hichi ambacho kuna mgogoro wa kisiasa visiwani humo baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Image caption Hits FM, ni miongoni mwa vituo vya radio vinavyofanya vizuri mjini Unguja

Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam Aboubakar Famau anasema kuwa meneja wa kituo hicho, ameeleza wachomaji hao walivyovamia majira ya usiku wa kuamkia leo, na kumwamrisha atoke nje kabla ya kuiwasha moto studio yao.

Aidha Mmiliki wa radio hiyo amesema wavamizi hao walikuwa wamejifunika nyuso zao.

Hits FM, ni miongoni mwa vituo vya radio vinavyofanya vizuri mjini Unguja, na pia ni miongoni mwa radio washirika wa BBC.

Image caption Mpaka sasa, lengo la wavamizi hao bado halijajulikana

Mpaka sasa, lengo la wavamizi hao bado halijajulikana, ingawa kitendo hicho kimefanyika wakati ambapo bado kuna mgogoro wa kisiasa unaendelea baina ya upinzani ambao unadai kushinda uchaguzi mkuu na chama tawala ambacho kinataka uchaguzi urudiwe.