Mwandishi wa habari auawa Somalia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwandishi wa habari auawa Somalia

Mwandishi mmoja wa habari wa kike ameaga dunia baada ya bomu kulipuka chini ya gari lake katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mwandishi huyo , Hinda Haji Mohamed, alikuwa akifanya kazi na shirika la habari la serikali.

Bomu hilo lililipuka karibu na ubalozi wa Uturuki mjini humo.

Hamna aliyedai kuhusika na shambulio hilo lakini kundi la kigaidi la Kiislamu la Al Shabaab limekuwa likiwalenga watu wengi katika mashambulio yake ya mabomu na risasi miaka ya hivi karibuni.