Wanawake Marekani sasa kwenda vitani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter ametangaza kuwa nafasi zote za kazi za kijeshi za kivita sasa zitakuwa wazi pia kwa wanawake wa Marekani.

Carter amesema huduma za kijeshi za Marekani hazitaweza tena kupunguza nusu ya watu wenye ujuzi na vipaji.

Amesema wanawake sasa wanaweza kuendesha magari ya deraya, mizinga na kuongoza askari wa nchi kavu kwenye mapambano.

Mpango huo wa kiistoria unakwenda kinyume na hoja ya mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa majeshi kwamba Kikosi cha askari wa majini wanaweza kuruhusiwa kuwatenga wanawake katika baadhi ya majukumu kwenye mapambano ya mstari mbele vitani.