Itagharimu pesa ngapi kutuma barua Mars?

Image caption Itagharimu pesa ngapi kutuma barua Mars?

Idara ya posta nchini Uingereza imepata jawabu kwa swali lisilo la kawaida kuhusu ni gharama kiasi gani itatumiwa kutuma barua kwenda sayari ya Mars.

Swali hilo liliulizwa na mtoto wa umri wa miaka mitano Oliver Giddings aliye na lengo la kuwa mwanasayansi wa anga za juu.

Haki miliki ya picha NASA
Image caption Sayari ya Mars

Kwa msaada wa NASA idara ya posta ilifanya makadirio ya kutuma barua kwenda kwa sayari hiyo na kupata kuwa itagharimu karibu dola 17,000.

Aliposikia hivyo alishangaa akisema kuwa pesa hizo ni nyingi kweli!

"Utahitaji stempu nyingi kweli kweli!" alisema Oliver kwa mshangao.