Watu 27 wauawa shambulio la mabomu Chad

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chad imekuwa ikisaidia Nigeria kukabiliana na Boko Haram

Watu 27 wamefariki na wengine kadha kujeruhiwa baada ya washambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Chad.

Maafisa wa usalama nchini Chad wanasema washambuliaji walilenga soko ambalo hufunguliwa kila wiki katika kisiwa cha Loulou Fou.

Shambulio hilo limetokea chini ya mwezi mmoja baada ya serikali ya Chad kutangaza hali ya hatari katika eneo la ziwa Chad.

Hii ilifanyika baada ya kuongezeka kwa mashambulio ya kigaidi kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram kutoka nchini jirani ya Nigeria.

Chad imekuwa ikisaidia Nigeria kukomboa maeneo mengi yaliyokuwa yametekwa na wapiganaji hao wa Kiislamu ambao wameua maelfu ya raia.