Je kuna nini kilomita 5 chini ya bahari ?

Haki miliki ya picha anisha shah
Image caption Je kuna nini kilomita 5 chini ya bahari ?

Wanasayansi wa Uingereza wanapanga kuchimba chini kabisa ya ardhi, katika bahari Hindi.

Lengo ni kufika chini zaidi ya tabaka za juu za ardhi, kwa mara ya kwanza.

Image caption Wanataka kuchunguza udogo kutoka ndani ya ardhi

Wanataka kuchunguza udogo kutoka ndani ya ardhi, na kuthibitisha yale yanayojulikana kuhusu umbo la ardhi.

Shughuli hizo zitachunguza iwapo kuna viumbe hai ndani zaidi ya ardhi kushinda vile vinavyojulikana.

Image caption Lengo ni kufika chini zaidi ya tabaka za juu za ardhi, kwa mara ya kwanza.

Zimefanywa juhudi mara kadha kuchimba ndani ya zaidi ya tabaka za juu za ardhi, lakini hazikufanikiwa.

Mwandishi wa BBC anayehusika na maswala ya sayansi, anasema kuchimba ardhi kina cha kilomita 5 chini ya bahari, ni kazi kubwa, na hadi sasa teknolojia imeshindwa.