Uchaguzi waanza Ufaransa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia nchini Ufaransa, wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa mashinani leo Jumapili

Raia nchini Ufaransa, wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa mashinani leo Jumapili, majuma matatu tu baada magaidi wa kundin la Islamic State waliposhambulia Paris, na kuwauwa watu 130.

Kura ya maoni inaonyesha kuwa chama cha mrengo wa kulia cha National Front, kina umaarufu mkubwa, katika uchaguzi huo hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa taifa hilo ambayo yanashuhudia kudidimia kwa uchumi, na anakotoka Marine Le Pen kama mgombea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Chama kinachopinga kuwepo kwa wakimbizi cha National Front cha Marine le Pen kinapigiwa upatu kushinda

Waandishi wa habari wanasema kuwa, chama kinacho ongozwa na Marine Le Pen kinatarajiwa kupata umaarufu mkubwa baada ya kubainika kuwa wahanga wawili wa kujitolea kufa waliingia barani Ulaya kama sehemu ya mmiminiko wa wahamiaji na wakimbizi waliopitia Ugiriki.

Shughuli za upigaji kura zinaendelea huku ulinzi mkali ukidumishwa, wakati huu ambapo tangazo la hali ya tahadhari lingalipo kote nchini Ufaransa.

Kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha mrengo wa kulia cha National Front, kimevutia wafuasi zaidi tangu mauaji hayo kutokea.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hollande anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha Marine Le Pen kinachopinga kuingia kwa wakimbizi

Chama hicho kinahusisha wageni na ugaidi.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, amejaribu kuvutia wapigaji kura kwa chama cha tawala cha Socialist, na ametoa wito watu wajitokeza kwa wingi kupiga kura.

Zaidi ya watu milioni 44 wanatazamiwa kushiriki zoezi hilo.