Mahasimu India na Pakistan wakutana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mahasimu India na Pakistan wakutana

Mazungumzo kati ya maafisa wa daraja za juu kati ya washindani wakuu na majirani, yaani India and Pakistan, yamefanywa miezi minne baada ya kuahirishwa.

Mataifa hayo hasimu yanajivunia kuwa na zana zenye teknolojia ya nuklia.

Baada ya mkutano huo uliofanywa mjini Bangkok, Thailand, maafisa wa idara za usalama za nchi hizo mbili, walisema, mazungumzo yao yalikuwa ya uwazi, kirafiki, na ya manufaa...na kwamba ushirikiano utasonga mbele.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ingawa waziri mkuu wa India, alimualika mwenzake wa Pakistan, katika sherehe za kuapishwa mwaka jana, uhusiano uliharibika baada ya hapo.

Ingawa waziri mkuu wa India, alimualika mwenzake wa Pakistan, katika sherehe za kuapishwa mwaka jana, uhusiano uliharibika baada ya hapo.

Watu kadha wameuwawa tangu wakati huo, katika mapmbano ya risasi mpakani.

India ilikuwa ikishinikiza kuwa mazungumzo lazima yajadili tu ugaidi - lakini taarifa iliyotolewa na pande zote inasema kuwa walishauriana kuhusu eneo lenye mzozo, la Kashmir, amani na usalama.