Mabunge 2 ya Libya kutatua mzozo wa kisiasa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabunge 2 ya Libya kutatua mzozo wa kisiasa

Mabunge mawili yanayopingana ya Libya, yamefikia makubaliano ya awali, yanayolenga kutatua msukosuko wa kisiasa nchini humo.

Katika mkutano uliofanywa Tunis, bunge linalotambuliwa kimataifa, lilitia saini msingi wa muafaka na bunge la jumla la taifa (General National Congress.)

Muafaka huo unakusudiwa kufikia serikali ya muungano na uchaguzi katika miaka miwili ijayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tangu marehemu kanali Gaddafi kupinduliwa na kuuwawa mwaka wa 2011, makundi tofauti yameteka sehemu nyingi za Libya

Makubaliano hayo ni mbali na zile juhudi za kupatanisha zinazofanywa na Umoja wa Mataifa, lakini Umoja wa Mataifa umekaribisha mazungumzo ya sasa.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na Libya, Martin Kobler, alisema huo ni msingi mzuri sana, kuwezesha kusonga mbele.

Tangu marehemu kanali Gaddafi kupinduliwa na kuuwawa mwaka wa 2011, makundi tofauti yameteka sehemu nyingi za Libya, na kundi la Islamic State, piya sasa linajitokeza huko.