Tabia nchi: Mapendekezo 2 yatolewa Ufaransa

Image caption Tabia nchi: Mapendekezo 2 yatolewa Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameidhinisha makubaliano kinzani yaliyoafikiwa na wapatanishi wa kimataifa, ili kukabiliana na ongezeko na mabadiliko ya tabia nchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafikiano kinzani yalikubaliwa Jumamosi, na yanajumuisha kupokelewa kwa maoni kutoka mataifa zaidi ya 150.

Akiongea mjini Paris mahala ambapo mkutano mkuu wa mbinu za kukabiliana na tabia nchi unafanyika Bwana Hollande, amesema kwamba mapendekezo hayo yatafaulu tu iwapo mataifa yatajizatiti na weka tofauti zao kando.

Maafikiano kinzani yalikubaliwa Jumamosi, na yanajumuisha kupokelewa kwa maoni kutoka mataifa zaidi ya 150.

Hata hivyo Bwana Hollande anasema kuwa ana matumaini suluhu na mwafaka wa pamoja utapatikana kufikia mwishoni mwa kongamano hilo katika kipindi cha juma moja lijalo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Ufaransa, ameidhinisha makubaliano kinzani yaliyoafikiwa na wapatanishi wa kimataifa

Rais Obama wa Marekani pia amezungumza na Rais Hollande kwa njia ya simu kujadili maendekezo yaliyoafikiwa katika mkutano huo wa mabadiliko ya mazingira.

Wajumbe kutoka mataifa 195 wanahudhuria kongamano hilo, linalofanyika katika eneo la Le Boughshe, karibu na mji wa Paris.