'Sauti' ya Mullah Mansour, yakanusha alikufa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mullah Mansour aliteuliwa miezi michache iliyopita, baada ya kujulikana kuwa muasisi wa kundi hilo la Taliban, Mullah Omar, alipofariki

Kundi la Taliban la Afghanistan, limetoa ujumbe wa sauti, ambayo wanasema, ni ya kiongozi wao, Mullah Akhtar Mansour, kukanusha madai kuwa amekufa.

Katika kanda hiyo ya sauti, mtu anakanusha ripoti zilizoenea kwamba aliuliwa nchini Pakistan juma lilopita, katika mapambano yaliyotokea mkutano na wapinzani wake ulipotibuka .

Wadadisi wa kundi hilo wanasema, sauti hiyo inaelekea kuwa ya Mullah Mansour.

Lakini maafisa waandamizi wa Taliban, wameliambia shirika la habari la AFP, wanafikiri ni ya uongo, au wanaamini kuwa alifariki kutokana na majeraha aliyopata.

Image caption Kuna kikundi chengine kimejitokeza na kiongozi wake tofauti.

Mullah Mansour aliteuliwa miezi michache iliyopita, baada ya kujulikana kuwa muasisi wa kundi hilo la Taliban, Mullah Omar, alipofariki miaka miwili iliyopita.

Kuna kikundi chengine kimejitokeza na kiongozi wake tofauti.