Ndege za Ulaya zashambulia wanajeshi wa Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za Ulaya zashambulia wanajeshi wa Syria

Ndege za muungano wa majeshi ya Ulaya zimeshambulia na kuua wanajeshi wanne wa Syria.

Kundi moja linalopigania haki za kibinadamu Syrian Observatory limesema wanajeshi wengine 13 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika kambi ya jeshi ya Saeqa.

Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Deir al-Zourambalo limekaliwa kwa asilimia kubwa na wanamgambo wa Islamic State Syrian Observatory for Human Rights inasema.

Iwapo madai hayo yatathibitishwa, basi hii ndio itakuwa tukio la kwanza la mashambulizi na mauaji ya majeshi watiifu kwa rais Bashar al Assad.

IS kulingana na Syrian Observatory for Human Rights yenye makao yake makuu nchini Uingereza inasema kuwa ndio inayotawala maeneo mengi katika jimbo hilo la Deir al-Zour.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Katika shambulizi lingine la majeshi ya Muungano ,mwanamke na mwanaye walifariki.

Katika shambulizi lingine la majeshi ya Muungano ,mwanamke na mwanaye walifariki.

Deir al-Zour ndio inayounganisha makao makuu ya Islamic State yaani Raqqa na maeneo yanayokaliwa na kundi hilo nchini Iraq.

Yamkini eneo hilo linavisima vingi vya mafuta ambayo inadhaniwa kuwa kitega uchumi kikubwa cha kundi hilo.

Majeshi ya muungano yamekuwa yakilenga Is kuanzia Septemba mwaka wa 2014.

Haki miliki ya picha AFP

Juma lililopita Uingereza iliidhinisha jeshi lake la angani kuishambulia IS nchini Syria.

Ufaransa kwa upande wake imeongeza maradufu mashambulizi ya ndege zake tangu wanamgambo hao kutekeleza shambulizi lililosababisha vifo vya watu 130 mjini Paris majuma matatu yaliyopita.