Upinzani waongoza uchaguzi wa kanda Ufaransa

EU Haki miliki ya picha AP
Image caption Chama cha National Front hupinga muungano wa EU na kuingia kwa wahamiaji Ufaransa

Kura zilizohesabiwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa kikanda nchini Ufaransa, zinaonyesha chama cha National Front Party kinaongoza katika matokeo kwa 30% ya kura zote zilizopigwa.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu kundi la kigaidi la wanamgambo wa dola ya Kiislamu la Islamic State kuua watu wapatao 130 mjini Paris mwezi uliopita.

Kufuatia kuongezeka kwa hofu dhidi ya mashambulio hayo, katika harakati za kupambana na wimbi la wahamiaji haramu,kutetea umoja wa Ulaya kumewekwa mstari wa mbele katika majimbo sita kati ya 13 ya Ufaransa.

Nacho chama cha serikali cha kisoshalisti, ambacho kimeshika nafasi ya tatu katika kura.

Chama hicho tawala kimelazimika kujiondoa katika uchaguzi wa awamu ya pili katika mikoa miwili katika jitihada za kukizuia chama cha National Front kuchukua ushindi maeneo hayo.