Kampuni ya Ujerumani yawapa wahamiaji ajira

Ujerumani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi inapungua Ujerumani

Siemens ni moja ya kampuni kubwa nchini Ujerumani ambayo imeamua kutoa ajira kwa wingi kwa vijana ambao wanawasili nchini humo kama wakimbizi.

Kampuni hiyo ambayo inaamini kuwa wahamiaji wanaoingia nchini humo huwa wana malengo makubwa zaidi katika ajira na hivyo ni muhimu kwa watu hao kupewa nafasi ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, wanahitajika sana Ujerumani ambako sehemu ya watu wenye umri wa juu inazidi kuongezeka.

Huku rais wa shirikisho linalowakilisha nchi katika viwanda vidogo na kati vya kibiashara wanasema wajumbe wake hawawezi kuwakubali wahamiaji hayo iwapo hawana uwezo wa kuongea Kijerumani.