Anglo American kuwafuta kazi 85,000

Image caption Anglo American kuwafuta kazi 85,000

Mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya uchimbaji madini Anglo American, imetangaza kufanya mabadiliko makubwa ili kupunguza gharama za utendakazi wake.

Kampuni hiyo imesema kuwa inapanga kutekeleza mabadiliko haya kuambatana na mfumuko wa bei ya bidhaa inazozalisha mbali na kupungua kwa utashi wa bidhaa zake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Anglo American - ambayo inachimba madini ya almasi, makaa ya mawe, chuma kama vile Platinum na shaba nyekundu, inapania kuwapunguza zaidi ya wafanyikazi 85,000.

Anglo American - ambayo inachimba madini ya almasi, makaa ya mawe, chuma kama vile Platinum na shaba nyekundu, inapania kuwapunguza zaidi ya wafanyikazi 85,000.

Aidha inapania kupunguza pia idara zake kutoka sita hadi tatu.

Pia itafutilia mbali gawio la malipo ya wawekezaji hadi mwisho ya mwaka ujao.

Image caption Shughuli kuu za kampuni hiyo ziko nchini Afrika Kusini, Australia na Marekani Kusini.

Shughuli kuu za kampuni hiyo ziko nchini Afrika Kusini, Australia na Marekani Kusini.

Wachanganuzi wanalaumu mdororo huo kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa kutoka China.

Kampuni zingine kubwa duniani kama vile Glencore na Rio Tinto, pia zimetangaza hasara baada ya kudorora kwa uchumi wa mteja wao mkuu China