Waandamanaji waachiliwa huru Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Waandamanaji waachiliwa huru Burundi

Takriban watu 100 waliokamatwa kwa makosa ya kuandamana mjini Bujumbura,Burundi kupinga muhula wa tatu wa rais Nkurunziza wameachiliwa huru.

Wanaamnika kuwa sehemu ya upinzani ulioanza kampeini ya kumzuia Pierre Nkurunziza asiwanie muhula wa tatu mwezi Mei.

22 walipewa kifungo cha nyumbani.

76 waliachiliwa huru baada ya mashtaka dhidi yao kufutiliwa mbali.

Image caption Gereza la Mpimba linatakriban mahabusu 4,000 wanaosubiri kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo kabla ya watu kuruhusiwa kwenda nyumbani walilazimika kuhudhuria darasa za uzalendo.

Gereza la Mpimba linatakriban mahabusu 4,000 wanaosubiri kufikishwa mahakamani.

Robo tatu kati yao hawajafunguliwa mashtaka.