Bendi ya Eagles of Death yarejea Paris

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bendi ya Eagles of Death yarejea Paris

Chini ya mwezi mmoja baada ya wanamgambo kushambulia tamasha katika ukumbi wa Bataclan mjini Paris na kuwaua watu 90 ,bendi ya Eagles of Death metal imetumbuiza tena mjini humo.

Bendi hiyo kutoka Marekani inayocheza miziki chapa Rock ilikaribishwa na kundi la U2 kutoka Ireland.

Waliimba wimbo wao maarufu wa 'I Love You All The Time' huku mashabiki wao wakijumuika nao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jumla ya watu 90 waliuwa kwenye tamasha ya bendi hiyo mjini Paris tarehe 13 mwezi uliopita.

Kiongozi wa bendi hiyo, Jesse Hughes alikuwa amevalia mavasi meupe.

Bendi hiyo ilisema kuwa inaupenda mji wa Paris na haitakoma kufanya tamasha zake mjini humo.

Jumla ya watu 90 waliuwa kwenye tamasha ya bendi hiyo mjini Paris tarehe 13 mwezi uliopita.