Tabia nchi yaunganisha mataifa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanaharakati wa mazingira

Umoja wa ulaya na mataifa 79 ya Afrika, eneo la Pacific na Caribbean wameungana kwa pamoja ili kuweza kufikia muafaka wa mazungumzo yanayoendelea mjini Paris.

Muungano huo umeamua kuwa na nia moja katika baadhi ya masuala yanayowatatiza huku wakitaka makubaliano yawekwe kisheria na kuwe na mabadiliko kila baada ya miaka mitano.

Lengo la mkutano huo ikiwa ni kupunguza ongezo la joto mpaka nyuzi joto moja na nusu. Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema Umoja wa Ulaya una nafasi kubwa wa kuweza kufikia makubaliano.

Waziri wa mambo ya nje nchini Ufaransa Lauren Fabius anasema rasimu mpya itawasilishwa leo hii.