Upinzani nchini Syria wakutana Saudi Arabia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Upinzani nchini Syria wakutana Saudi Arabia

Makundi ya upinzani nchini Syria yanatarajiwa kukutana nchini Saudi Arabia katika jitihadi za kuunganisha makundi hayo yanayopigania kumuondoa madarakani rais Bashar al Assad.

Mkutano huo ambao utafanyika mjini Riyadh una lengo la kubuniwa kwa kundi ambalo litajadiliana na serikali kuamua ikiwa mazungumzo ya amani yataendelea.

Makundi yaliyoalikwa ni pamoja na kundi la Free Syrian Army linaloungwa mkono na marekani pamoja na makundi mengine ya kiislamu yanayoungwa mkono na Saudi Arabia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kundi la Islamic State na lile lenye uhusiano na Al Qaeda la Nusra Front pia nayo yametengwa.

Hata hivyo kundi la wakurdii nchini Syria halijaalikwa na hivyo linafanya mkutano wake.

Vilevile ,Kundi la Islamic State na lile lenye uhusiano na Al Qaeda la Nusra Front pia nayo yametengwa.