UN: Demokrasia imo mashakani DR Congo

Wafungwa DRC Haki miliki ya picha
Image caption Umoja wa Mataifa unasema watu wengi wamefungwa na kuwekwa mahabusu bila hatia DRC

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa fursa ya kuwepo kwa demokrasia inaendelea kufifia katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi.

Ripoti iliochapishwa na kitengo cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu imebaini kwamba visa vya mauaji ya kiholelea, vitisho vya mauaji, kuwakamata na kuwafunga watu kiholela vinavyofanywa na wanajeshi vimeongezeka tangu uliopanza mchakato wa uchaguzi mwezi Januari.

Lakini Waziri wa mambo ya ndani nchini ameikosoa ripoti hiyo akisema haina malengo yoyote na haielezi wazi ni wapi visa hivyo vilitendeka.

Haki miliki ya picha
Image caption Umoja wa Mataifa unasema wanajeshi wa DRC walitekleleza mauaji ya jumla na ya kikatili

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inasema tume ya uchaguzi DR Congo huenda isitekeleze majukumu yake kutokana na kuwepo kwa vikwazo vya uhuru.

Shirika hilo linasema kulikuwa na visa vya mauaji ya kikatili ya watu wapatao 21 na visa 649 vya kuwakamata watu na kuwaweka mahabusu kinyume cha sheria kati ya mwezi Januari na Septemba.

Wengi waliotendewa unyama huo walikuwa ni waandamanaji, wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa mashirika ya kiraia waliopinga kucheleweshwa kwa uchaguzi wa urais.