Wakulima waaswa wapunguze antibiotics

Nguruwe Haki miliki ya picha Nick Turner NPL
Image caption Dawa za maambukizi zaanza kushindwa kuwatibu wanyama

Wakulima wametakiwa kupunguza kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kukabiliana na viini zinazotumiwa katika kilimo, kwa sababu ya tisho la dawa hizo kwa afya ya binadamu, ripoti imesema.

Baadhi ya maambukizi yamefikia kiwango cha karibu kutotibika, kutokana na matuimizi ya dawa hizo kupita kiasi.

Zaidi ya nusu ya zile zinazotumika kote duniani hutumiwa kwa mifugo, na mara nyingi hutumiwa kuwafanya wakue haraka.

Uchunguzi juu ya uwezo wa vimelea wa kutotibiwa umetoa wito yawekwe malengo mapya ya kiwango cha dawa zinazotumiwa.

Haki miliki ya picha SCIENCE PHOTO LIBRARY
Image caption Wanasayansi waonya hakuna uwezo wa tiba zaidi ya Antibiotics

Tisho kubwa la matumizi ya kupita kiasi ya dawa katika kilimo lilitangazwa nchini Uchina mwezi uliopita.

Wanasayansi wameonya kuwa dunia haijafikia ''enzi ya matumizi ya zaidi ya dawa za kukabiliana na viini" baada ya kubaini kuwa vimelea vya magonjwa vimeshindwa kuangamizwa na dawa ya dawa aina ya colistin - dawa ambayo kwa kawaida hutumiwa pale nyinginge zinaposhindwa kutibu.

Hali hii ilionekana kuongezeka katika wanyama kabla ya kupatikana miongoni mwa wagonjwa wa hospitalini.