Chanjo ya Dengue kutumika Mexico

Image caption Mbu

Mamlaka za afya nchini Mexico zimeruhusu matumizi ya chanjo ya kwanza duniani dhidi ya homa ya dengue inayosababishwa na mbu.

Chanjo hiyo ilivumbuliwa na kundi la watafiti wa maabara ya dawa nchini Ufaransa iitwayo, Sanofi, yapata miaka ishirini iliyopita.

Mpaka sasa, inakadiriwa kuwa watu zaidi ya elfu arobaini wanatarajiwa kupokea chanjo hiyo nchini Mexico.

Chanjo hiyo iitwayo Dengvaxia itatolewa tu kwa watoto wenye umri zaidi ya miaka 9, na watu wazima walio na umri chini ya miaka 45, ambao wanaishi katika maeneo yanayoshambuliwa na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Dengue unaongoza kwa wagonjwa kulazwa hospitalini katika nchi za Latin Amerika na nchi za Asia. Ugonjwa huo hatari umekwisha ua watu zaidi ya elfu ishirini mwaka jana pekee.