Taliban wavamia uwanja wa ndege Afghanistan

Uwanja wa ndege wa Kandahar
Image caption Taleban wasema wamewauwa askari kadhaa wa serikali ndani ya uwanja huu

Kumekua na taarifa zamapigano makali baina ya vikosi vya serikali na vile vya Taliban ndani ya uwanja wa ndege wa Kandahar nchini Afghanistan, ambao ni mji mkuu wa eneo la kusini mwa nchi.

Taleban wanasema kuwa wamewauwa askari kadhaa, wa serikali na wa kigeni, lakini hakuna duru huru zilizothibitisha madai haya, na hali taarifa majeruhi haziko wazi.

Haki miliki ya picha bb
Image caption Msemaji wa gavana wa jimbo la Kandahar asema Taleban walikabiliwa na upinzani wa majeshi ya serikali

Mseamji wa gavana wa jimbo hilo amesema kua wapiganaji kadhaa waliweza kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa Kandahar, lakini walikutana na ulinzi mkali uliowarejesha nyuma.

Mtandao wa Taliban uliwaelezea washambuliaji wake kama wakujitolea mhanga kufa kwa ajili ya dini, wakimaanisha walijilipua kwa mabomu.

Image caption Mashambulio ya hivi karibuni yalilenga eneo la Wapashtun

Hili ni shambulizi baya lililofanywa na Taleban katia eneo lake la Wapashtun, kinyume na mashambulio yake ya hivi karibuni ambayo waliyoyafanya katika eneo lisilokaliwa na Wapashtun la kaskazini.

Wamefanya mashambulio haya licha ya kugawanyika kwa kundi hilo katika makundi mawili, na licha ya uvumi kwamba kiongozi mpya wa kundi hilo aliuawa hivi karibuni.