Vatican: Uzazi wa mpango suluhu ya mazingira

Kardinali Peter Turkson Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kardinali Peter Turkson anasema kanisa katoliki halijawahi kukataa mpango asilia wa uzazi

Mmoja wa wakuu wa kanisa katoliki amesema kuwa mpango wa uzazi unaweza ''kutoa suluhu'' ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kardinali Peter Turkson, ambae ni mshauri mkuu wa Papa Francis wa masuala ya hali ya hewa, ameiambia BBC kuwa kanisa halijawahi kupinga mpango wa uzazi wa njia asilia.

Akizungumza mjini Paris, Kardinari huyo alittoa wito wa kuwepo kwa makubaliano thabiti yatakayolinda nchi zinazoathirika zaidi.

Anasema mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha maafa makubwa kwa viumbe hai.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kanisa katoliki limeongeza ushiriki wake katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa

Cardinal Turkson anaaminiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuandaa muswada wa Papa Francis wa mabadiliko ya hali ya hewa al maarufu "Laudato Si".

Hivi karibuni kanisa katoliki liliidhinisha ushiriki wake mkubwa katika suala la mazingira, likiwahamasisha waumini kushiriki matembezi ya dunia kuhusu uhifadhi wa mazingira kabla ya kuanza kwa mkutano wa dunia wa Mazingira COP21.

Kanisa katoliki ia limeongeza ushiriki wake katika mchakato wa mazungumzo yanayohusu masuala ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa.