Merkel ashinda tuzo ya Time ya mwaka 2015

Merkel Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ujerumani imewapokea wahamiaji karibu milioni moja mwaka huu

Jarida la Time limemtaja Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa "Mtu mashuhuri wa Mwaka” 2015.

Jarida hilo limetaja mchango wake katika kutatua mzozo kuhusu wahamiaji Ulaya pamoja na mgogoro wa madeni wa Ugiriki kama moja ya mambo yaliyochangia kutawazwa kwake.

Kadhalika, jarida hilo limetaja kuingia kwa Urusi nchini Ukraine.

Bi Merkel ametoa “uongozi wa busara katika ulimwengu ambao umepungukiwa”, mhariri wa jarida hilo Nancy Gibbs ameandika.

Kiongozi wa kundi la wapiganaji linalojiita Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi ametajwa kuwa wa pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Donald Trump, anayesaka tiketi ya kuwania urais Marekani kupitia chama cha Republican.

Bi Merkel amejiunga na washindi wa awali wakiwemo Adolf Hitler, Joseph Stalin, Mahatma Gandhi, Winston Churchill na Richard Nixon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Merkel alisaidia kutatua mzozo wa wahamiaji Ulaya

Tuzo ya mwaka jana ilikabidhiwa matabibu waliosaidia kukabilina na mkurupuko wa Ebola Afrika Magharibi.