Wajumbe wagawanyika mkutano wa Paris

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Ufaransa, Francis Holand

Tofauti kubwa kati ya mataifa tajiri na yale yanayoendelea imejitokeza katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Paris pale majukumu ya kazi yalipoanza kugawanywa usiku kucha katika rasimu ya makubaliano iliyoandaliwa na wenyeji Ufaransa.

Waziri Laurent Fabius amesema kuwa ana uhakika watamaliza wakiwa na mafanikio lakini kazi zaidi inahitajika kufanyika kabla ya mkutano huo kuisha siku ya Ijumaa.

Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanadai mapendekezo yaliyotolea yanatoa mwanya kwa mataifa tajiri kukwepa majukumu yao wakati wakiwa wanaziacha nchi hizo zinazoathirika bila msaada wowote.

Mataifa mengine wanasema rasimu hiyo itashindwa kufikia malengo labda tu kama watatuma ujumbe ulio wazi ambao utawasukuma kuja na suluhisho ambalo litaendana na kipindi fulani.

Akizungumza na waandishi wa habari, mjumbe maalumu wa Marekani kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Todd Stern, ameainisha baadhi ya vipengele ambavyo anahisi ni muhimu:

Haki miliki ya picha Reuters

"Tunahitaji kuwa na mzunguko wenye utaratibu mzuri kila baada ya miaka mitano ili nchi zetu ziweze kuwasiliana na kufanya marekebisho au kuifanya iende na wakati katika malengo tuliyojiwekea na hayo yanahitajika kufanyika mapema .Tunaitaji malengo ya muda mrefu ,tunahitaji zaidi ya nyuzi joto mbili,tunahitajika kuwa na makubaliano ambayo yana nguvu na yaliyowazi ili kila mtu afahamu nini tunachokifanya."

Kamishna wa umoja wa ulaya kuhusu nishati na mabadiliko ya tabia nchi, Miguel Arias Canete, amesema bado kuna fursa ya kufanyiwa maboresho kwa waraka wa makubaliano:

"Ujumbe ulioko kwenye maandishi uko wazi ,hauna haja ya kuuwekea msisitizo au kuwa na nia Zaidi ya tulionayo.Sisi sote hapa tumefanya kazi kubwa pamoja ili kuweza kuyafanya malengo yetu yakubalike ingawa bado tuna safari kubwa mbele yetu."