US na UK zashauriwa kutoiuzia silaha Saudia

Image caption Vita nchini Yemen

Shirika la Amnesty International limeilaumu Saudi Arabia na washirika wake kwa kushambulia shule nchini Yemen.

Amnesty inasema kuwa tangu muungano unaoongozwa na Saudi Arabia uanzishe mashambulio ya angani mwezi Machi, zaidi ya shule 20,000 zimeharibiwa huku robo ya shule hizo zikiharibiwa kabisa.

Kwenye ripoti mpya, Amnesty inataka Marekani na Uingereza kusita kuiuzia silaha Saudi Arabia ikisema kuwa silaha hizo zinatumiwa kwa vitendo vinavyokiuka sheria za kimataifa nchini Yemen.

Zaidi ya watu 6000 wanaripotiwa kuuawa katika mzozo nchini Yemen.