Wakimbizi wa Syria wawasili Canada

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Canada akiwalaki wakimbizi kutoka Syria

Ndege ya kwanza ya kijeshi iliyowabeba wakimbizi kutoka Syria ambao wamepewa hifadhi nchini Canada, kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo, imetua katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Toronto.

Watu 163 kutoka Syria, walikaribishwa katika uwanja huo wa ndege na Waziri Mkuu, Justin Trudeau.

Serikali ya Bwana Trudeau, ilichaguliwa mwezi Oktoba na kukubali kuchukua wakimbizi 25,000 kutoa syria ifikapo mwishoni ma mwaka huu.

Kufuatia mashambulizi yaliyotokea mjini Paris, ilibadili mpango wake na wengine wanatarajiwa kuwasili mapema mwaka ujao.