Putin aagiza majeshi yakabili tishio Syria

Putin Haki miliki ya picha AFP
Image caption Putin amenukuliwa mara kadha akisema Uturuki itajuta kudungua ndege ya Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wanajeshi wa Urusi kuchukua “hatua kali” dhidi ya hatari zozote zinazojitokeza Syria.

Hatari zozote zinazokabili majeshi yake zinafaa “kuangamizwa mara moja”, amewaambia wakuu wa jeshi.

Bw Putin hakufafanua zaidi lakini Uturuki na Urusi kwa zimekuwa zikizozana kufuatia kuangushwa kwa ndege ya kivita ya Urusi na majeshi ya Uturuki.