Mwanamfalme wa Saudia amshutumu Trump

Talala Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bin Talal amesema Donald Trump hawezi kushinda urais Marekani

Mwanamfalme Alwaleed bin Talal wa Saudi Arabia amemshutumu mgombea urais wa chama cha Republican Marekani Donald Trump kwa tamko lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.

Mwanamfalme huyo, ambaye ndiye mtu tajiri zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, amesema Bw trumo anafaa kuacha azma yake ya kutaka kuwa rais kwa sababu hawezi kushinda.

"Unaletea aibu chama cha Republican na Marekani kwa jumla," ameandika Bin Talal kwenye Twitter.

Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, alikuwa amependekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani kwa sababu za kiusalama.

Hii ni baada ya wanandoa wawili Waislamu kufyatua risasi na kuwaua watu 14 mjini San Bernardino, jimbo la California.

Amejibu matamshi hayo ya Bw Talal kwa kumuita mwanamfalme ”mjinga” na kumtuhumu kwa kutaka kufanya anachosema ni kutumia “pesa za baba” kudhibiti wanasiasa wa Marekani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Trump amesisitiza kwamba hataacha kuwania urais Marekani

"Hutaweza kufanya hivyo nikichaguliwa," amemjibu Trump kupitia Twitter.