Aliyewalazimisha 150 kuavya mimba akamatwa

Image caption Serikali ya Colombia inasema kuwa thuluthi moja ya wanamgambo wa FARC ni wanawake

Polisi wa Uhisipania wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kwa madai kuwa aliwalazimisha wapiganaji wanawake katika kundi la waasi la Colombia, FARC, kuavya mimba.

Serikali ya Colombia inataka mwanamume huyo, Hector Arboleda Buitrago, ambaye amekuwa akifanya kazi ya uuguzi mjini Madrid kusafirishwa hadi nchini humo kujibu mashtaka.

Mnambo Ijumaa Colombia ilisema kuwa zaidi ya wanawake 150 walitoa ushahidi kueleza jinsi mtu huyo alivyowaavya mimba.

Mkuu wa Sheria nchini Colombia, Eduardo Monteleagre, alisema kuwa kuna ushahidi kuwa kundi hilo la FARC lilikuwa na sheria za kuwalazimisha wanawake kutoa mimba ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kupigana katika maasi nchini humo.

Mwanamke mmoja aliyefanikiwa kujiopndoa kutoka kwa kundi hilo alimwmbia mwandishi wa habari wa BBC mjini Bogota Natalio Cosoy kuwa ilikuwa bahati kuruhusiwa kujifungua.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa waasi wa FARC na rais wa Colombia walipokutanishwa katika mazungumzo ya amani nchini Cuba

Mwanamke huyo anasema kuwa alilazimishwa kuavya mimba mara 5.

Kundi la waasi wa FARC wamekuwa wakiendesha maandamano kwa miaka 50 hivi.Hata hivyo kwa sasa wanafanya mazungumzo ya amani na Serikali ya Colombia nchini Cuba.