Miaka 5 jela kwa ulanguzi wa Kakakuona, China

Image caption Miaka 5 jela kwa ulanguzi wa Kakakuona, China

Mwanamume mmoja raia wa China amehukumiwa jela miaka 5 kwa kujaribu kulangua kakakuona 'Pangolins' 26 na kuwaingiza nchini humo.

Ripoti kutoka China zinasema kuwa Tang alifumaniwa akijaribu kuwalangua wanyama hao 26 kwenye gari lake la uchukuzi akitokea nchio jirani ya Vietnam.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aidha ilibainika kuwa 20 kati ya wanyama hao walitokea Malaysia.

Kwa mjiu wa uchunguzi wa polisi Tang alilipwa ilikuwalangua wanyama hao kutoka Malaysia.

Aidha ilibainika kuwa 20 kati ya wanyama hao walitokea Malaysia.

Kakakuona ni moja kati ya wanyama wa porini wanaoingizwa nchini China kinyume cha sheria.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kwa mjiu wa uchunguzi wa polisi Tang alilipwa ilikuwalangua wanyama hao kutoka Malaysia.

Nyama ya mnyama huyo anasemekana kuwa tamu mno na yenye uwezo wa kutibu magonjwa kadhaa .

Wanaharakati wanasema huenda hii ni ishara kuwa serikali ya China imeanza kuitikia mwito wa kupamabana na ulanguzi wa wanyama pori na bidhaa zinazotokana na wanyama pori kama vile meno ya tembo na pembe ya kifaru.