Kerry ajaribu kuishawishi Urusi kuhusu Syria

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry yuko mjini Moscow kwa mazungumzo kuhusu njia za kumaliza vita vya wenyewe vya zaidi ya miaka minne nchini Syria .

Mazungumzo baina ya Bwana Kerry na mwenzake wa Urusi , Sergey Lavrov, yanalenga kuondoa tofauti kati ya Urusi na Marekani hususan kuhusu makundi yanayofaa kushirikishwa katika mazungumzo ya amani ya Syria.

Urusi ambayo inaunga mkono rais , Bashar al-Assad --inasema kuwa mkutano wa hivi karibuni wa upinzani wa serikali ya Syria haukuwa na uwakilishi na ulijumuisha kile alichokiita makundi ya kigaidi .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Urusi --inasema kuwa mkutano wa hivi karibuni wa upinzani ulijumuisha makundi ya kigaidi .

Mwandishi wa BBC anasema Bwana Kerry atajaribu kuandaa fursa ya mazungumzo ya mataifa tajiri duniani kuhusu mzozo wa Syria baadaye wiki hii mjini New York.

Bwana Kerry anatarajiwa kukutana na rais Vladimir Putin baadaye.

Urusi inamuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad na inasisitiza kuwa inataka awe uongozini katika kipindi cha mpwito.

Marekani na washirika wake wanapinga al Assad kuendelea kuwepo kuwa uongozini.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi ilianza kampeini ya kuwaadhibu makundi ya kiislamu mnamo mwezi wa Septemba

Urusi ilianza kampeini ya kuwaadhibu makundi ya kiislamu mnamo mwezi wa Septemba hatua ambayo iliinusuru uongozi wa Assad na kuwaudhi sana mataifa yanayompinga yakiwemo uturuki ambayo ilidungua ndege ya kijeshi ya Urusi.