Lomu hakuacha pesa zozote alipofariki

Lomu Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lomu alichezea New Zealand mechi 63

Mchezaji nyota wa mchezo wa raga kutoka New Zealand Jonah Lomu alikuwa mkarimu sana na hakuacha pesa zozote alipofariki.

Sasa, wakfu umeanzishwa wa kuchangisha pesa za kusaidia watoto na familia yake.

Lomu alifariki Novemba akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kuugua ugonjwa wa figo tangu 1995.

Afisa mkuu mtendaji wa Chama cha Wachezaji raga wa New Zealand Rob Nichol amesema Lomu alikuwa mkarimu sana.

"Alikuwa mnyenyekevu na mtu mwenye kuweka siri zake na aliamua kutoomba usaidizi au kuwa mzigo kwa wengine. Licha ya ugonjwa wake, alikuwa na matumaini kwamba angeweza kuendelea kukidhi mahitaji ya familia yake.”

Hata hivyo, Nichol amesema familia ya Jonah haijaomba msaada.

Image caption Lomu alifana sana akichezea All Blacks

Lomu alifunga trai 37 katika mechi 63 alizochezea New Zealand kati ya 1994 na 2002.

Alilazimika kuacha kucheza na akafanyiwa upasuaji na kupandikizwa figo nyingine mwaka 2004. Hata hivyo, figo hiyo iliacha kufanya kazi 2011.

"Kufuatia kifo chake, Jonah sasa hawezi kutunza watoto wake, kulipia malezi yao, mahitaji mengine na elimu.”