Hoteli iliyoshambuliwa Mali kufunguliwa

Mali Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu 22 waliuawa kwenye shambulio hilo

Hoteli iliyoshambuliwa katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mwezi jana itafunguliwa tena leo.

Watu wenye silaha walishika mateka wageni 170 kwa saa tisa katika hoteli ya Radisson Blu, na kuua watu 22 na kujeruhi wengine 14.

Polisi na wanajeshi wa Mali, wakisaidiwa na vikosi vya usalama kutoka nje, waliingia kwenye hoteli hiyo na kuwaua washambuliaji.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kupitia Twitter kwamba hoteli hiyo itafunguliwa.