Mataifa ya Kiislamu 34 kupambana na ugaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mataifa ya Kiislamu 34 kupambana na ugaidi

Saudi Arabia imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu wa kukabiliana na ugaidi.

Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mataifa ya ghuba yanakabiliwa na shinikizo kufanya juhudi zaidi katika vita dhidi ya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria

Wajumbe wa muungano huo ni mataifa ya kiarabu, Afrika na Asia Kusini .

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia , Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kua muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na Afghanstan .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri wa ulinzi wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ndiye aliyetangaza muungano huo

Hata hivyo kuna taarifa chache kuhusu namna kikosi hiki kitakavyotekeleza majukumu yake.

Mataifa ya ghuba yanakabiliwa na shinikizo kufanya juhudi zaidi katika vita dhidi ya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria

Oroda ya mataifa katika muungano huo

 • Saudi Arabia,
 • Bahrain,
 • Bangladesh,
 • Benin, Chad,
 • Comoros,
 • Djibouti,
 • Misri,
 • Gabon,
 • Guinea,
 • Ivory Coast,
 • Jordan,
 • Kuwait,
 • Lebanon,
 • Libya,
 • Malaysia,
 • Maldives,
 • Mali,
 • Morocco,
 • Mauritania,
 • Niger,
 • Nigeria,
 • Pakistan,
 • Palestina,
 • Qatar,
 • Senegal,
 • Sierra Leone,
 • Somalia,
 • Sudan,
 • Togo,
 • Tunisia,
 • Uturuki,
 • Milki za Kiarabu
 • Yemen.