Argentina na fedha za kigeni

Haki miliki ya picha AP
Image caption Peso ya Argentina

Argentina inasitisha masharti ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambayo yameimarisha sarafu ya taifa hilo.

Masharti hayo yaliimarisha sarafu ya Peso kwa miaka minne iliopita.

Waziri wa fedha wa nchi hiyo amesema kuwa mfumo wa zamani uliweka masharti ya ukuaji wa uchumi na kwamba hataruhusu wafanyabiashara kununua dola nyingi kwa kiwango wanachotaka.

Raia wa kawaida wa Argentina bado atakabiliwa na masharti hayo.