EU wajadili uanachama wa Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bendera ya Uingereza na ya Umoja wa Ulaya

Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesema wako tayari kufikia mapatano ya kuiwezesha Uingereza kusalia katika Muungano huo.

Hata hivyo viongozi hao wanaokutana mjini Brassels, wamesisitiza kuwa makubaliano yoyote hayapaswi kuvunja kanuni za muungano wa Ulaya.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kumekua na mafanikio, lakini akasema bado kuna kazi ngumu inayowasubiri mbele yao.

Rais wa Muungano wa Ulaya, Donald Tusk amesema kuwa viongozi wengine walielezea hofu zao kuhusu mpango wa Uingereza wa kukabiliana na malipo ya kijamii ya wahamiaji wa Muungano wa Ulaya suala ambalo wengi wanaliona kama Ubaguzi.

Mkutano huo pia utajadili mzozo wa wahamiaji na makubaliano kuhusu haja ya kuimarisha mipaka ya nje ya Muungano wa Ulaya.