ECOWAS yapanga kupiga marufuku mtandio

Mtandio Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanawake waliovalia mtandio unaofunika uso wametumika kujitoa mhanga Nigeria

Muungano wa nchi wanachama wa Afrika Magharibi ECOWAS umezitaka mataifa wanachama kupiga marufuku mtandio unafunika hadi uso, ili kuzia mashambulio yanayotekelezwa na wanawake wa kujitoa mhanga.

Mkutano wa ECOWAS uliofanyika mjini Abuja Nigeria umesema mtandio huu wa hadi uso unayumbisha operesheni za maafisa wa usalama katika kuwanasa wahalifu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ecowas inasema walinda usalama wanashindwa kuwatambua wahalifu waliovalia mtandio unaofunika uso

Kaskazini mwa Nigeria wapiganaji wa Boko Haram wamekua wakiwatumia wasichana wadogo na wanawake kutekeleza mashambulio ya kujitoa mhanga.

Walipuaji wamekua wakivalia mavazi mapana na kuficha mabomu ndani ya mavazi hayo. Kundi hilo pia limetumia mbinu hiyo katika mataifa ya Cameroon, Chad na Niger ambayo yanashiriki katika operesheni dhidi ya Boko Haram.