Trump amshukuru Putin kwa kumsifia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Donald Trump amesifiwa na Rais wa Urusi Vladmir Putin

Mmoja wa wagombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump amesema kwamba amekaribisha vyema kauli ya Rais wa Urusi Vladmir Putin kumhusu.

Bwenyenye huyo wa Marekani amemsifia Putin kama kiongozi anayeheshimiwa nchini mwake na hata katika ngazi ya kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump ni miongoni mwa wanaoongoza kwenye kinyang'anyiro cha Republican

Putin alimtaja Trump kama mtu wa kupendeza na mwenye ujuzi mkubwa wakati wa hotuba yake kwa taifa. Viongozi hao wawili wanajulikana kwa lugha wanayotumia, japo hawafahamiani binafsi.

Donald Trump ni miongoni mwa wanaoongoza kwenye kura ya maoni katika kinyang'anyiro cha kuipeperusha bendera ya chama cha Republican kwenye uchanguzi mkuu mwaka ujao.