Uchaguzi wa Hispania,matokeo yasubiriwa

Image caption Raia wa Hispania wakiwa katika mstari wa kusubiri kupiga kura.

Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Hispania yanaashiria kuwa vyama viwili vimepata karibu theluthi moja ya viti bungeni, na kufanikiwa kuutikisa mfumo wa vyama viwili ya siasa nchini humo.

Chama maarufu kinachoongoza nchini humo kinatabiriwa kupoteza wingi wa viti vyake ingawa bado kinafurukuta katika ushindi , kikifuatiwa na chama cha kijamaa.baada ya kupambana na chama chenye ushawishi mkubwa, Podemos,ambacho kinatabiriwa ushindi karibu kwa asilimia ishirini ya viti.

Kambi nyingine mpya , ya chama cha wananchi cha kiliberali, nacho kinatarajiwa kunyakua viti vingi.matokeo rasmi ya uchaguzi huo mkuu, ambao ni mkali kuwahi kutokea katika kipindi cha miongo kadhaa, yanatarajiwa kutolewa.